![]() |
| Picha/uhondodaily.com |
Upendo wa kuigiza ni hali ambayo mtu humzidishia mwenzake upendo, zawadi, sifa na uangalizi wa kupita kiasi kwa muda mfupi, si kwa sababu ya mapenzi ya dhati, bali kwa lengo la kumpumbaza au kumdhibiti kihisia. Mara nyingi huonekana mwanzo wa uhusiano ambao kila kitu kinaonekana kizuri kupita kiasi, lakini baadaye hutibuka na kugeuka mzigo mkubwa kwa mhusika.
Tofauti na mapenzi ya kweli yanayokua hatua kwa hatua, upendo wa kuigiza hutokea ghafla. Mhusika hufanya kila njia kuonyesha kama vile amepata mapenzi ya maisha yake, lakini ukweli ni kwamba anaandaa mazingira ya kumtegemea au kumtii. Hii ni mbinu inayotumika mara nyingi na watu wenye hulka za udhibiti, ubinafsi mkubwa (narcissism) au kwenye mahusiano yaliyojengwa kwa tamaa.
Mifano ya Upendo Kutoka Kwa Mtu Anayeigiza
1. Ahadi za Haraka
Mtu anakwambia ndani ya siku chache tu: “Wewe ndiye niliyekuwa nikisubiri maisha yangu yote, nataka tuwe pamoja milele”.
2. Simu na Ujumbe Mfululizo
Anakupigia simu mara nyingi mno, anatuma meseji kila dakika, na anataka kujua ulipo au unafanya nini kila muda.
3. Zawadi Kubwa Bila Mpangilio
Baada ya siku chache tu, anakuja na zawadi kubwa za gharama kubwa bila sababu ya msingi.
4. Kuharakisha Hatua za Uhusiano
Anaanza kuzungumza kuhusu ndoa, kuishi pamoja au hata kupata watoto kabla hamjajuana vizuri.
5. Kubadilika Baada ya Kumuamini
Mara unapoanza unapoanza kuwekeza mapenzi yako kwake, ghafla anapunguza upendo, anakulaumu, au anataka uishi kwa masharti yake.
Madhara ya Upendo wa Kuigiza
1. Huzuni na kuchanganyikiwa kwa sababu ya kupokea mapenzi ya ghafla kisha unaondolewa ghafla.
2. Kumtegemea kihisia mtu anayekuchezea.
3. Kupoteza kujiamini kwa sababu kila kitu kinaonekana anataka kiwe kwa masharti yake.
4. Kujiingiza kwenye uhusiano hatari unaoweza kuharibu hali yako ya kisaikolojia na kimwili.
Jinsi ya Kujilinda na Upendo wa Kuigiza
1. Usikubali kuharakishwa kuingia kwenye uhusiano mzito bila kumjua mtu vizuri.
2. Angalia kama vitendo vyake vinaendana na maneno yake.
3. Jitunze kihisia: kumbuka thamani yako haitokani na kupokea zawadi kubwa au sifa zisizoisha.
4. Weka mipaka ya wazi na usiogope kusema “hapana” unapohisi shinikizo.
Hitimisho
Upendo wa kuigiza (love bombing) siyo ishara ya mapenzi ya kweli bali ni mbinu ya kupumbaza. Mapenzi ya kweli yanajengwa kwa uvumilivu, heshima, na uaminifu, si kwa haraka na shinikizo. Ni muhimu kutambua ishara zake mapema ili kuepuka kuingia kwenye mtego wa mahusiano hatarishi.
👉 Je, umewahi kukutana na mtu aliyekupa upendo wa ghafla kupita kiasi kisha baadaye akabadilika ghafla?

Post a Comment